Uwezeshaji wa kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi ni juhudi za makusudi zinazoanzishwa na Serikali ili kuwasaidia wananchi wake waweze kushiriki vizuri katika shughuli za kiuchumi. Uwezeshaji unaweza kufanyika kwa kupitia Sera sahihi, Sheria sahihi, kukuza ujuzi wa wananchi, upatikanaji wa mitaji nafuu, taarifa sahihi za masoko na programu mahsusi ambazo zinazompa fursa mwananchi ya kushi...
Kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kupitia utekelezaji wa sera, sheria, mikakati, programu na miongozo kuhusu maendeleo ya sekta binafsi na uwezeshaji kiuchumi
Kuweka mazingira yatakayowezesha watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi rasmi
Kuratibu majadiliano kuhusu uwezeshaji kiuchumi na maendeleo ya sekta binafsi;