Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofaidika kupitia programu ya Enhanced Integrated Framework (EIF) iliyoanzishwa na kuratibiwa na Shirika la Biashara la Dunia (World Trade Organisation – WTO). Programu hii inalenga kusaidia nchi zinazoendelea ambao ni wananchama wa WTO kukabiliana na changamoto za uzalishaji ikiwemo miundombinu hafifu, sera na sheria, na uwezo mdogo wa sekta binafsi kuzalisha bidhaa...
Kuimarisha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kufanikisha biashara na uwekezaji wa viwanda katika maeneo yao.
Kuimarisha Tafiti na uchambuzi wa Sera katika biashara
Kuimarisha ushindani wa biashara ndogo na kati katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa
Tanzania ilianza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya programu ya EIF kwa Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kuendeleza Biashara (Capacity Development for Trade (CDMT) EIF – Tier 1 Phase 1 na Phase II) kuanzia mwaka 2013–2016. Mradi huu ulilenga kujenga uwezo wa kitaasisi wa kuandaa na kusimamia Sera, Mikakati na Mipango ya Maendeleo ya Biashara (Institutional Capacity Building).
Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa programu ya EIF. Utekelezaji wa awamu ya pili uliolenga kusaidia nchi kutekeleza miradi ya kukuza Biashara (Productive Capacity Building) ulianza.
Katika awamu hii mradi wa Tier II Phase I unaojulikana (Strengthen MSMEs Capacity to Improve Competitiveness in Domestic, Regional and International Markets for Selected Value Chains) ulianza kutekelezwa kuanzia 2020 kwa pande zote, Tanzania Bara na Zanzibar
Wanufaika wakubwa wa mradi ni Wizara zinazosimamia sekta ya biashara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta binafsi hasa biashara ndogo na kati katika maeneo ya mazao ya mnyororo wa thamani yaliyochaguliwa. Maeneo hayo ni Mikoa ya Kigoma, Singida, Mara na Simiyu, Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba.
i) Mkoa wa Singida Wilaya ya Itigi
Mradi huu umelenga kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali katika mazao ya Nyuki (Asali, Nta, Gundi, Sumu) na kuwajengea Viwanda vidogo viwili Itigi Mjini na Mwamagembe vyenye Vifaa vya kisasa vya kuchakata mazao hayo ili kuongeza thamani katika mnyororo wa mazao hayo ili yaweze kuingia katika ushindani wa soko la kitaifa, Kikanda na Kimataifa.
ii) Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Busega na Mkoa wa Mara Wilaya ya Bunda
Mradi umelenga kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali wa Mboga mboga na Matunda na kuwajengea kituo cha kukusanya na kuhifadhi mbogamboga na matunda (collection center) pamoja na mashine za kuchakata na kukaushia mbogamboga matunda.
iii) Mkoa wa Kigoma Wilaya ya Uvinza na Kigoma Vijijini.
Mradi huu umelenga kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali katika zao la Chikichi, kuwajengea viwanda vidogo viwili vya kusindika mafuta ya kula ya mawese na vifaa vya kisasa katika Wilaya ya Uvinza na KigomaVijijini ili kuongeza thamani katika mnyororo wa zao hilo na kuingia katika ushindani wa soko la kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Zao la Chikichi linatumika kutengeneza mafuta ya kula na vipodozi (sabuni, losheni, manukato).
iv) Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mradi huu umelenga kutoa mafunzo na kuwawezesha wakulima wa zao hilo boti ya kusafirishia Mwani na vifaa vya kisasa vya kilimo ili kuongeza thamani katika mnyororo wa zao hilo na kuingia katika ushindani wa soko la kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Zao la Mwani linatumika kama chakula na kutengeneza bidhaa za dawa, mbolea na vipodozi (sabuni, losheni, manukato)
v) Mkoa wa Kaskazini Unguja
Mradi huu umelenga kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali wa zao la dagaa na eneo la huduma bora (Common Facility) la kusarifia (Processing) na Mashine ya Vifungashio (Packaging), ili kuongeza thamani katika mnyororo wa zao hilo ili liweze kuingia katika ushindani wa soko la kitaifa, Kikanda na Kimataifa