Wizara ya Viwanda na Biashara (MIT) ilianzisha Kitengo cha Kaizen Tanzania (TKU) kusambaza falsafa ya KAIZEN kote nchini. Falsafa hiyo inalenga kutumia kwa ufanisi rasilimali zilizopo, pamoja na mbinu bunifu na jumuishi katika kupunguza gharama zisizo za lazima viwandani ili kuongeza tija na ubora kwenye mnyororo wa thamani.