Tanzania ni moja ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zitakazonufaika na Mradi wa EU-EAC Market Access Upgrade Programme (MARKUP). Mradi huo unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya ili kusaidia nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza matakwa ya Mkataba na Itifaki za Jumuiya ya Afrika Mashariki.