Sekta ya Viwanda vidogo na Biashara ndogo inasimamiwa na Kitengo cha Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Kitengo hiki kinajukumu kuu la kusimamia na kuratibu Maendeleo ya Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo kupitia sera, mikakati, mipango na program mbalimbali
Kuandaa, kurejea, kufuatilia na kuwezesha utekelezaji wa Sera, mikakati, mipango na program za maendeleo ya sekta ya SME
Kuwezesha, uhitimu (SME graduation), ukuaji, urasimishaji na maendeleo ya viwanda vijijini
Kupanga mikakati ya kuwezesha ushiriki wa makundi malaalum katika ujasiriamali na maswala mtambuka
Kuratibu mipango na (initiatives) za wadau wanaoshiriki katika maendeleo ya sekta
Kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na zisizo za kifedha kwa wajasiriamali
Kuwezesha upatikanaji wa sehemu mahsusi za kufanyia kazi kwa SMEs.
Kukuza ujasiliamali na kuendeleza Ujuzi