Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) umekuwa ukijulikana kama “BLUEPRINT”. MKUMBI unalenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini (Blueprint for Regulatory Reform to Improve Business Environment). MKUMBI unalenga kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kupunguza au kuondoa na kuboresha changamoto mbalimbali katika ufanyaji biashara kama majukumu ya taasisi yana...
Kuanzisha na kutekeleza shughuli za kuhamasisha na kuhakikisha taratibu bora za udhibiti, utoaji leseni na vibali
Kuhakikisha majukumu ya mamlaka za udhibiti yanayoingiliana yanaondolewa na yanayofanana yanaunganishwa
Kukuza uwazi katika mamlaka za udhibiti kwa kuweka mifumo ya TEHAMA inayotoa taarifa, huduma na taratibu zinazohitajika kwa umma kwa wakati
Kuanzisha mfumo madhubuti wa ufuatiliaji na tathimini ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa maboresho yanayopendekezwa
i) Maboresho yanayofanywa na mamlaka za udhibiti yasilenge kuongeza mapato bali kukidhi gharama za utoaji huduma.
ii) Sheria, Kanuni na Taratibu zilenge kutekeleza sera ya biashara, ushindani, kumlinda mlaji na huduma za umma.
iii) Kukuza ushindani wa kimkakati wenye usawa, tija na ubunifu kwa kupunguza tozo na ada.
iv) Majukumu ya mamlaka za udhibiti yanayoingiliana yaondolewa na yanayofanana yaunganishwe.
v) Ukusanyaji wa mapato utumie nyezo rahisi na rafiki kwa kutumia mifumo ya dirisha moja na vituo vya pamoja.
vi) Udhibiti uwe kwa lengo la kuendeleza sekta husika au uzalishaji.
vii) Kuwa na mifumo ya udhibiti yenye uhakika, endelevu na inayotabirika.
viii) Kuhakikisha kuwa maboresho ya kupunguza kanuni hayaondoi mamlaka ya udhibiti.
ix) Kanuni zote zitakazotungwa zifanyiwe tathmini ya athari ya udhibiti kabla ya kuidhinishwa kutumika.
x) Chagamoto za kiutendaji ndani na baina ya mamlaka za udhibiti zitatuliwe.
The Government approved the implementation of the Blueprint for regulatory reforms to improve the business environment in 2018, and the Blueprint Action Plan (BAP) in 2019
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA NA KUWEKA MAZINGIRA BORA NA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA
Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini (Blueprint) ili kuvutia uwekezaji na kuwezesha ufanyaji biashara
Wito kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuhakikisha wanakuwa Walezi wa Jumuiya za Wafanyabiashara
Dkt. Kijaji: Uwekezaji, Vwanda na Biashara ndio msingi wa maendeleo wa Taifa lolote Duniani