Sekta ya Viwanda inasimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Viwanda chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Idara hii ina jukumu kuu la kusimamia, kuendeleza, na kuweka mazingira bora ya ukuaji endelevu wa sekta ya viwanda nchini.
Kutoa na kuratibu misaada ya kiufundi katika uundaji, mapitio na kuwezesha utekelezaji wa sera, mikakati, mipango, program na sheria za kuhamasisha maendeleo ya viwanda
Kuwezesha uundaji na uimarishaji wa vyama vya kisekta na kitaifa vya wazalishaji viwandani
Kuhamasisha na kuratibu shughuli za utafiti na maendeleo ya viwandani na kushirikiana na taasisi za mafunzo, sayansi na teknolojia ili kukuza rasilimali watu za stadi zinazofaa.
Kuwezesha utekelezaji wa programu maalum chini ya vitengo vya KAIZEN, TDU, na IIU ili kuboresha maendeleo ya viwanda
Kufuatilia na kutathmini utendaji wa viwanda na utekelezaji wa miradi ya viwanda
Kuwezesha mchakato wa kitaifa wa mashauriano ili kukuza maendeleo ya viwanda nchini
Kutoa misaada ya kiufundi ili kuwezesha uwekezaji katika sekta ya viwanda
Kuandaa taarifa za kina za sekta ya viwanda