Mtangamano wa Biashara inasimamiwa na Idara ya Mtangamano wa Biashara chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Kitengo hiki kinajukumu kuu la Kutambua na kukuza fursa za biashara katika ushirikiano wa kibiashara, baina ya nchi rafiki, kikanda na kimataifa
Kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kurejea utekelezaji wa Sera, mikakati, mipango, programu, sheria na kanuni zinazohusu mtangamano wa biashara
Kutambua na kukuza fursa za biashara katika ushirikiano wa kibiashara, baina ya nchi rafiki, kikanda na kimataifa
Kuandaa msimamo wa nchi katika majadiliano ya kibiashara baina ya nchi rafiki, kikanda na kimataifa kwa kushirikiana na wadau wengine
Kuratibu utekelezaji wa majukumu ya mikataba katika majadiliano ya kibiashara baina ya nchi rafiki, kikanda na kimataifa
Sera ya Biashara kwa Uchumi Shindani na Ukuaji wa Mauzo ya Nje 2003