Sekta ya Biashara na Masoko inasimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Biashara chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Idara hii inajukumu kuu la kuweka Mfumo wenye tija na ufanisi katika biashara na masoko ili kukuza uchumi wa viwanda
Kuandaa, kufuatilia, kutathmini na kurejea utekelezaji wa sera, sheria na kanuni za biashara na masoko
Kuwezesha upatikanaji wa bidhaa na huduma na usambazaji wa taarifa za biashara na masoko
Kufanya utafiti wa masoko, intelijensia ya masoko na uchambuzi wa mnyororo wa thamani kwa bidhaa na huduma kwa masoko ya ndani na nje
Kusimamia ukuaji wa biashara na masoko na kuhakikisha ufuasi na utendaji wa taasisi za udhibiti
Kuwezesha sekta binafsi kujengewa uwezo wa kushiriki katika biashara na masoko
Kuwezesha na kuendeleza Miundombinu na Vifaa vya Masoko
Kuwezesha uwekezaji katika Biashara
Sera ya Biashara kwa Uchumi Shindani na Ukuaji wa Mauzo ya Nje 2003