Habari
WAKULIMA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA FURSA ZA VIWANGO VYA MAZAO VYA DUNIA- MBWASI
📌Afungua kikao cha 45 cha kimataifa cha wataalamu wa dunia wa viwango vya nafaka na kunde(
📌kufungua fursa na kunufaika na masoko ya Kimataifa
Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi amesema, Wakulima nchini wanakwenda kunufaika na uwepo wa viwango vya ubora wa mazao wa dunia ambao unakwenda kujadiliwa na nchi wananchama wa ISO Duniani.
Amesema hayo wakati akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Waziri Salum katika Ufunguzi wa Mkutano wa 45 wa kamati ndogo ya kiufundi ya nchi wanachama wa Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) unaojadili kuhusu nafaka na mikunde Jijini Dar es Salaam.
Mbwasi amesema,uwepo wa Mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania na Shirika la Viwango nchini (TBS) kwani Shirika linashiriki mkutano huo kikamilifu katika uandaaji wa viwango na si kupokea viwango kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania na ulimaji katika viwango vyake ili kuuza kwenye masoko ya nje na Kimataifa kwa bidhaa za jamii ya mikunde na nafaka.
Ameongeza kuwa uwekaji wa viwango vya mazao hayo utakwenda kuwanufaisha wakulima nchini kujua viwango vipi vya kimataifa vimewekwa kuhusu hali ya nafaka na mazao jamii ya mikunde yanatakiwa katika masoko ya kimataifa.
Aidha amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania kwani viwango vinamgusa mkulima anayehifadhi anayesafirisha nje,anayetumia na wenye viwanda.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Dkt. Candida Shirima amesema ,matarajio ya Tanzania kupitia Shirika la Viwango Viwango Tanzania ni kwamba wataalam watawasilisha mahitaji ya watanzania katika mkutano huo ili kujadiliwa na kuweza kuzingatiwa katika viwango vinavyoandaliwa kwa kuhakikisha usalama wa bidhaa, kulinda wananchi na kuwezesha biashara nchini na masoko ya Kimataifa.
