Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Muundo wa Wizara

MUUNDO WA WIZARA 

Wizara ya Viwanda na Biashara ina Idara sita (6) Vitengo saba (7) na Taasisi 13. Taasisi hizo zina umuhimu wa kipekee katika kuendeleza na kufungamanisha Sekta ya Viwanda na Biashara na sekta nyingine nchini.

IDARA NA VITENGO VYA WIZARA 

Wizara ina Idara za Maendeleo ya Viwanda; Maendeleo ya Biashara; Mtangamano wa Biashara: Viwanda Vidogo na Biashara ndogo; Sera na Mipango; na Utawala na Maendeleo ya Rasilimali Watu. Vitengo vya Wizara ni ; Fedha na Uhasibu; Ukaguzi wa Ndani; Huduma za Sheria; Usimamizi wa Ununuzi; Mawasiliano Serikalini; TEHAMA na Ufuatiliaji na Tathimini.

TAASISI ZILIZOCHINI YA WIZARA 

Taasisi zilizo chini ya Wizara zinajumuisha Mashirika matano (5) ambayo ni; Shirika la Maendeleo la Taifa (National Development Corporation - NDC), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Small Industries Development Organization - SIDO), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania Industrial Research Development Organization - TIRDO), Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (Tanzania Engineering and Manufacturing Design Organization – TEMDO) na Shirika la Viwango Tanzania (Tanzania Bureau of Standards - TBS).

Aidha, kuna Wakala mbili (2) ambazo ni Wakala wa Vipimo (Weights and Measures Agency - WMA) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Business Registrations and Licensing Agency – BRELA). Pia kuna Mamlaka moja (1) ambayo ni Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tanzania Trade Development Authority – TANTRADE).

Vilevile Wizara ina Mabaraza mawili (2) ambayo ni Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal - FCT) na Baraza la Taifa la Utetezi wa Haki ya Mlaji (National Consumers Advocacy Council - NCAC) linalosimamiwa na FCC 

Wizara pia ina kituo kimoja (1)  ambacho ni Kituo cha Zana za Kilimo na Utafiti Vijijini (Centre for Agricultural Mechanisation of Rural Technology - CAMARTEC).

Wizara inasimamia Chuo kimoja (1) cha Elimu ya Biashara (College of Business Education - CBE), Tume moja (1) ya Ushindani (Fair Competition Commission - FCC) na Bodi moja (1) ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (Warehouse Receipt Regulatory Board -WRRB