Kitengo Mawasiliano Serikalini
Lengo
Kutoa ushauri wa kitaalamu wa masuala ya habari, mawasiliano na utoaji wa taarifa kwa vyombo vya habari na kwa wananchi.
Majukumu
- Kuandaa na kusambaza taarifa na machapisho mbalimbali (Vipeperushi, Jarida na Makala) yanayoelimisha Umma kuhusu Sera, Sheria, programu, shughuli na maboresho yanayotekelezwa na Wizara;
- Kuratibu mikutano ya Wizara na vyombo vya habari na Wizara;
- Kuwasiliana na wananchi pamoja na vyombo vya habari kuhusu masuala yote yanayoihusu Wizara;
- Kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Wizara;
- Kuratibu maandalizi ya nyaraka mbalimbali za Wizara na za kisekta kwa ajili ya warsha na mikutano;
- Kuratibu maandalizi na utengenezaji wa Makala (print and electronic) na magazeti ya Wizara; na
- Kusimamia shughuli zinazendeshwa na Maktaba ya Wizara.