Tathimini na Ufuatiliaji
Kitengo cha Tathimini na Ufuatiliaji
Lengo
Kusimamia, kuratibu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera, mipango, bajeti, programu, miradi na Maeneo muhimu ya Matokeo ya Kitaifa (NKRA).
Majukumu
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera, Mpango Mkakati wa Muda wa Kati, mipango ya mwaka, bajeti, programu na miradi kwa kuzingatia Mfumo wa Taifa wa Mipango;
- Kufuatilia na kutathmini Maeneo muhimu ya Matokeo ya Kitaifa (NKRA) ya Wizara;
- Kufanya tathmini za matokeo za mipango, programu na miradi chini ya Wizara;
- Kuandaa na kutekeleza muundo (M&E framework) na mfumo (system) wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara;
- Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya tathmini;
- Kuandaa taarifa za mara kwa mara za M&E kuhusu NKRA za Wizara;
- Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala na Maelekezo ya Serikali;
- Kufuatilia na kutathmini utendaji wa Wizara kwa vipindi maalum na wa dharura;
- Kufuatilia utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara;
- Kuratibu mapitio ya utendaji wa taasisi / Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Utendaji wa Taasisi za Umma (PIPMIS); na
- Kuhifadhi na kusimamia takwimu za Wizara.
