Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Uhasibu na Fedha

Lengo

Kusimamia matumizi sahihi ya fedha na kutunza taarifa za fedha za Wizara

Majukumu

  • Kusimamia matumizi sahihi ya fedha za Serikali;
  • Kushauri Menejimenti kuhusu taratibu, kanuni na sheria za matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia ukusanyaji mapato ya Serikali kwa Fungu 44 na 60;
  • Kukusanya na kuwasilisha maduhuli ya Serikali kwa niaba ya Mlipaji Mkuu wa Serikali;
  • Kusimamia na kuhasibu fedha zote za Wizara zinazotolewa na Serikali na wafadhili kwa mujibu wa Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Tanzania;
  • Kuandaa taarifa mbalimbali za Fedha na kihasibu ikiwa ni pamoja na Hesabu za Wizara (Fungu 44 na 60), Taarifa za Robo na nusu mwaka, majibu ya hoja za ukaguzi, kwa kufuata sheria kanuni na miongozo na kuwasilisha sehemu husika kwa wakati; na
  • Kuandaa na kutunza taarifa mbalimbali za fedha ikiwa ni pamoja madeni ya Wizara na kuwasilisha Hazina.