Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Majukumu ya Wizara

Wizara ya Viwanda na Biashara imeundwa kwa mujibu wa Tamko la Serikali Na. 685 la tarehe 19 Desemba, 2025 na kupewa majukumu kupitia Tamko la Serikali Na. 686 la tarehe 19 Desemba, 2025 na kupewa majukumu mahsusi ya kisekta kama ifuatavyo:-

  1. Kusimamia maendeleo ya Viwanda na Biashara;
  2. Kusimamia maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo;
  3. Kuendeleza miundombinu ya viwanda;
  4. Kusimamia miliki bunifu;
  5. Kusimamia masuala ya ushindani wa haki;
  6. Kusimamia vipimo, viwango na ubora;
  7. Kusimamia intelijensia ya masoko na uhamasishaji wa biashara;
  8. Kusimamia usajili wa biashara;
  9. Kufanya kazi na Taasisi za kimataifa zinazohusiana na Viwanda na Biashara;
  10. Kuimarisha na kuendeleza ufanisi wa rasilimali watu katika Wizara; na
  11. Kusimamia Idara, Taasisi, programu na miradi chini ya Wizara.