Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Utawala na Rasilimali Watu.

Lengo

Kutoa ushauri wa kitaalamu na huduma katika masuala ya  Usimamizi wa Utawala na Raslimali watu kwa Wizara  

Majukumu

  • Kutafsiri Kanuni za Utumishi wa Umma, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma na Sheria za Kazi
  • Kujenga na Kuboresha Mahusiano kazini na kushughulikia Maslahi ya Watumishi ikiwemo Afya, Usalama Kazini, Michezo, kuratibu ushiriki wa Michezo, Bonanza  na Maadhimisho ya Kitaifa;
  • Kushughulikia masuala ya safari, Itifaki, usafiri, maji, umeme, simu, huduma za Masijala na Mapokezi na kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo ujenzi na ukarabati wa majengo, upatikanaji wa vitendea kazi na matengenezo ya mitambo;
  • Kuandaa bajeti ya Mishahara, kupandisha vyeo na kuthibitisha watumishi kazini;
  • Kushughulikia Ajira za Mikataba na Kuwabadilisha vyeo watumishi;
  • Kuandaa na kusimamia mpango wa mafunzo na kuratibu mafunzo elekezi kwa watumishi wapya;
  • Kuendesha mashauri ya nidhamu kwa watumishi na kuidhinisha likizo za watumishi; na
  • Kuratibu na kusimamia Upimaji Utendaji Kazi kwa Watumishi