Usimamizi wa Ununuzi (PMU)
Lengo
Kutoa usahuri wa kitaalamu na huduma katika ununuzi utunzaji na ugavi wa bidhaa na huduma kwa Wizara
Majukumu
- Kushauri Menejimenti juu ya masuala yote yanayohusu ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali
- Kuratibu na Kusimamia ununuzi;
- Kutunza na kusimamia mali za Wizara;
- Kuandaa Mpango wa Ununuzi wa wizara; na
- Kuandaa viwango vya bidhaa (Specification) pamoja na kusimamia viwango vilivyowekwa kwa bidhaa na huduma zote zinazonunuliwa.