Sera na Mipango
Lengo
Kutoa huduma na ushauri wa kitaalamu katika uaandaaji, Utekelezaji, Ufuatiliaji na tathimini wa Sera za maendeleo.
Majukumu
Idara hii ina majukumu yafuatayo
- Kuratibu maandalizi ya Sera za Wizara, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathmini ya matokeo ya utekelezaji wa Sera zote;
- Kuchambua sera za sekta nyingine, Kuzioanisha na malengo ya sekta ya Viwanda na Biashara pamoja na kutoa muongozo;
- Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara pamoja na Taasisi zake (Internal Resource Mobilization);
- Kuratibu Masuala ya Programu na Miradi kutoka kwa Wadau wa Maendeleo (External Resource Mobilization);
- Kufanya ufuatiliaji na tathmini na kuandaa taarifa za utekelezaji wa Wizara ikiambatana na maandalizi ya Hotuba ya Bajeti na Taarifa za mwaka za Hali ya Uchumi; na
- Kuhamasisha na kuwezesha utoaji wa huduma wa Sekta Binafsi katika Wizara