Ukaguzi wa Ndani
Lengo
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Afisa Masuhuri kuhusu usimamizi sahihi wa raslimali
Majukumu
- Kukagua na kutoa taarifa kama kuna udhibiti wa kutosha kwenye makusanyo, utunzaji namatumizi ya rasilimali fedha za ofisi;
- Kukagua na kutoa taarifa juu ya usahihi wa hesabu na taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na ofisi;
- Kupitia na kutoa taarifa juu ya shughuli au mipango ya ofisi ili kuona kama inaendana na malengo na madhumuni ya uanzishwaji wa ofisi;
- Kuandaa Mpango kazi na Mpango mkakati wa ukaguzi; na
- Kuandaa na kusimamia mipango ya ukaguzi.