Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Lengo Kuu
Kitengo cha TEHAMA kina jukumu kubwa la kuiwezesha wizara kufanya kazi zake kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Majukumu
- Kupitia Sera za TEHEMA kwa ajili ya maboresho yake
- Kusimika miundombinu ya TEHAMA pamoja na kusimamia matengenezo yake.
- Kutoa mafunzo juu ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA.
- Kushauri matumizi sahihi ya vifaa vya TEHAMA na kusimamia manunuzi ya vifaa hivyo(hardware&software)
- Kutoa msaada wa kitaalam kwenye matumizi ya vifaa na mifumo ya TEHAMA.
- Kushauri juu ya usimikaji wa mifumo mipya ya TEHAMA.
- Kukusanya takwimu na taarifa za viwanda, biashara na masoko ili na kuziweka kwenye mfumo (kanzidata)