Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. Dotto Biteko ,aagiza Viwanda vyote vilivyopo katika halmashauri zao kushiriki kikamilifu katika maonesho ya Kimataifa.


 

 

Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Doto Biteko (Mb) ambaye pia ni Waziri wa Nishati kwaniaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Philip Isdor Mpango ameagiza Mikoa na Halmashauri zote chini kuhakikisha viwanda vyote vilivyopo katika halmashauri zao kushiriki kikamilifu katika maonesho ya Kimataifa.
 
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa Maonesho ya pili ya Viwanda Kimataifa nchini Tanzania (TIMEXPO-2024) yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam kuanzia leo septemba 26,2024 na kufikia tamati oktoba 02,2024.
 
Dkt. Biteko amesema ushiriki wa viwanda hivyo utasaidia kuonesha bidhaa wanazozalisha ili bidhaa hizo ziweze kutafutiwa masoko ya ndani na nje ya nchi yakiwemo ya ukanda wa EAC na SADC kwa lengo la kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma za Tanzania nje ya nchi.

Aidha amezitaka taasisi zinazotoa huduma kwa wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika maonesho mbalimbali ili kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo.
 
Vilevile Dkt. Biteko ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kuendelea kuhakikisha maonesho yanayoandaliwa yanakuwa na tija na kuvifanya viwanda vya ndani kuwawanufaika ili waweze kupata soko na kuhakikisha mamlaka za ubora nchini zinasimamia ipasavyo ubora wabidhaa zote .

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na BiasharaMhe.Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa maonesho hayo yamelenga kuwaunganisha wazalishaji na wafanyabiasharakutoka Tanzania na Mataifa ya nje ili kubadilishana uzoefuwa teknolojia na kujifunza na hiyo yote ni jitihada za Rais waJamhuri ya Muungano wa Tan zania Mhe.Dkt.Samia SuluhuHassan ya kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wa nje.
 
Pia Mhe.Kigahe amesema maonesho hayo ya Viwanda ni ya pili ambapo yameonesha mwitikio mkubwa ukilinganisha na maonesho ya kwanza ya mwaka 2023 ambapo yalikuwa na washiriki 79 na sasa wamefikia zaidi ya washiriki 250 kutoka ndani na nje ya Nchi.