Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. Hashil Abdallah: WMA endeleeni kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewataka mameneja vipimo katika mikoa kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa wananchi kwa kuwa malalamiko yamekua mengi kuhususiana na Taasisi hiyo.

Ameyasema hayo  Mkoani Morogoro Februari 18, 2023 katika kikao kazi kilichowakutanisha mameneja vipimo nchini.

Aidha, amewasisitiza kutokufanya  ukaguzi kwa kutumia nguvu badala yake  watengeneze mazingira ya kuwaelewesha wafanyabiashara umuhimu wa kuzingatia vipimo katika bidhaa na amewataka kujirekebisha yale ambayo yanalalamikiwa,

Pia amewataka kusimamia utekelezaji wa sheria hizo kuwa wezeshi, ili mazingira ya ufanyaji biashara nchini yaendelee kuwa bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara  ya Maendeleo ya Biashara, Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Bw. Sempeho Manongi amewataka   mameneja hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Pia amewataka mameneja mikoa hao kuhakikisha mazingira ya kufanya biashara nchini yanayafanyika kwa haki kwa kuwa taasisi hiyo inashughulika bidhaa zinazozalishwa ndani na nje ya nchi.

Pia aliitaka taasisi hiyo kufanya kazi kwa uwazi, ili kuepuka vitendo visivyofaa ambavyo vimekua vinaleta malalamiko kwa jamii.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Stelle Kahwa amehaidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa kwa lengo la kusimamia usahihi wa vipimo katika sekta mbalimbali ili wananchi waweze kupata bidhaa zenye vipimo sahihi pasipo kupunjwa.

Kadhalika amesema wakala itaendelea kufanya kaguzi mbalimbali za kushtukiza kwa lengo la kuendelea kuwalinda wananchi na wafanyabiashara wote nchini.