Habari
DKT.JAFO AZINDUA WIKI YA SHERIA KISARAWE
DKT.JAFO AZINDUA WIKI YA SHERIA KISARAWE
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye amezindua Wiki ya Sheria na kupokea maandamano kwenye Viwanja vya Chanzige,Kisarawe Mkoani Pwani.
Ameyasema hayo Januari 25, 2025 wakati akizindua Wiki ya Sheria kwa Wilaya ya Kisarawe ambapo ameitaka Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe kuendelea kuwasikiliza wananchi kwa ukaribu ili kuondoa kero zao ili kila mmoja apate haki zake na kuendelea kupeleka kesi kwa haraka.
Aidha dkt.Jafo amempongeza Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Bi.Emmy Amob Nsangalufu kwa kuendesha kesi mbalimbali zenye malalamiko wilayani humo na kutambua mchango wake wa kutatua mashauri mbalimbali ya wananchi.
Vilevile Dkt. Jafo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe.Petro Magoti na kusema kuwa ni kiongozi wa mfano nchini Tanzania kutokana na umahiri wake wa kuwatumikia na kuwafikia wananchi na kutumia Ofisi yake kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Wakati huohuo Dkt. Jafo amewasisitiza wananchi wa Kisarawe kushiriki kwenye elimu ya Sheria watakayoipata na kuhakikisha kila mmoja anamlinda mwenzake katika masuala ya haki na usawa.
Nae Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Kisarawe Emmy Amon Nsangalufu amesema kuwa kila mwaka Mahakama ya Tanzania imeweka utaratibu wa kuadhimisha Wiki ya Sheria ambayo Inacanya kila mwanamchi atambue kuwa ni jukumu la Mahakama kuhakikisha inawafikia wananchi kwa wakati pale inapobidi na kuongeza kuwa Katika wiki hiyo wanahakikisha wanatoa elimu ya sheria kwa Wananchi itakayosababisha kupata haki zao.