Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

DKT SERERA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUENDANA NA KASI YA TEKNOLOJIA


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera amewataka watumishi wa Umma kuendelea kuwa wabunifu kwa kujielimisha mara kwa mara ili waendande na kasi ya maendeleo ya Teknolojia.

Dkt. Serera ameyasema hayo Oktoba 21, 2025 jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO).

Ameongeza kuwa, kila mtumishi wa Umma ameajiriwa baada ya kufanya usaili lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuwa ujuzi alioajiriwa nao ukawa umeshapitwa na wakati. Ni vizuri kukawa na mpango wa kuendelea kuwaruhusu watumishi kwenda kusoma.

Aidha, maarifa anayokuwa ameyapata yatasaidia kuinua ufanisi wa kiutendaji mahala pa kazi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo, Mhand.Prof. Sylvester Mpaduje amewashukuru Viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuwa na utamaduni wa kutembelea Taasisi zake na kurahisisha mfumo wa kuendelea kuwahudumia wananchi kwa wakati.