FCC ongezeni nguvu katika kudhibiti bidhaa bandia mipakani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe, Balozi Dkt. John Sembachawene ameisisitiza Tume ya Ushindani (FCC), kuongeza nguvu katika udhibiti wa bidhaa bandia hususani kipindi hiki ambacho wanajipanga kuingia katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA) kutimiza azma ya Serikali ya kukuza uchumi na biashara.
Mhe. Balozi Dkt. Simbachawene ameyasema hayo Septemba 24, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara yake katika Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) ili kujifunza, kujua shughuli za Taasisi hiyo na kuweza kufahaminiana na watendaji wa Tume hiyo.
Aidha, Balozi Dkt. Simbachawene ameitaka Taasisi hiyo kuhakikisha wanaweka nguvu kubwa katika kudhibiti bidhaa zinazoingia nchini kupitia mipaka yote nane Bandari ya Dar es Salaam, Tunduma, Holili, Tarakea, na Namanga
zisiwe bidhaa feki kwa kuwa Tanzania inatekeleza Mkataba wa AFCFTA ambao umeruhusu bidhaa kutoka Nchi yoyote ya Afrika kuweza kuingia nchini ili kuwalinda walaji na kulinda uchumi kwa ujumla.
“Tunapowalinda walaji tunajilinda na sisi ambao tunatumia bidhaa na tunalinda uchumi kwa maana ya kwamba tunapofungua soko ushindani utakua mkubwa, bidhaa zitatoka Uganda, Kenya, Malawi hivyo bidhaa hizo kama tusipokuwa na FCC iliyokuwa imara tutajikuta bidhaa za Tanzania zinaweza kukosa soko”
Mbali na hayo aliwapongeza watumishi wote wa FCC kwa ujumla kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuwalinda walaji na kuitaka FCC kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili waweze kuelewa kwa undani kuhusu masuala ya bidhaa bandia na jinsi ya kuzidhibiti.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Bw. William Erio ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na Bunge kwa kuridhia kupitishwa kwa Marekebisho ya Sheria ya Ushindani 2003 iliyifanyiwa marekebisho madogo mwaka 2019/ 2020-2021 ”
ambayo italeta ufanisi zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za kukuza na kushajiisha uchumi wa nchi kupitia biashara