Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI YATATUA CHANGAMOTO YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Jidith Kapinga (Mb) amesema Serikali imechukua hatua za kukabiliana na changamoto ya wafanyabiashara wageni waliokuwa wanafanya biashara katika soko la Kariakoo ambapo kamati (Viongozi wa Wizara na wadau) ilikutana na viongozi wa wafanyabiashara na wadau mbalimbali na kuchukua maoni ya namna ya kuboresha kanuni na taratibu za soko la Kariakoo na kuweka mpango wa kumaliza tatizo hilo.

Hayo yamebainisha katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo Aprili 25, 2026 jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine Waziri Kapinga ameongeza kuwa Lengo la Serikali ni kuendelea kukuza Biashara katika Soko la Kariakoo na wafanyabiashara ni sehemu muhimu sana ya uchumi wa nchi na moja ya malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ni mitaji asilimia 70 itoke kwenye sekta binafsi.