Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KUWEZESHA SEKTA BINAFSI


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwezesha sekta binafsi kuendelea kukua na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika Hafla ya Kazi na Bunifu za Biashara kwa Vijana (Career Fair 2026) lililobeba kaulimbiu ya “Ubunifu na Ujuzi kwa Vijana; Msingi wa Ukuaji wa Biashara na Viwanda Tanzania,” amesema Career Fair ya mwaka huu itatoa nafasi kwa vijana kujifunza kutoka kwa wataalamu, kuonesha vipaji vyao, kupata taarifa za fursa mbalimbali, kujenga mtandao na kujiandaa vizuri kwa mahitaji ya maisha ya sasa na baadaye.

Aidha, amesema vijana wengi huona fursa za biashara baada ya wengine kuanzisha, hivyo kuamua kuiga badala ya kuja na ubunifu wao. Amesema hali hiyo huwafanya wakose faida ya kuingia sokoni mapema, jambo linaloweza kuathiri mafanikio yao katika biashara. ‎