Habari
MAANDALIZI YA MKUTANO WA MAWAZIRI KATI YA TANZANIA NA ZAMBIA YAKAMILIKA
Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Biashara (Joint Trade Committee – JTC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zambia yamekamilika kufuatia kuhitimishwa kwa kikao cha Kamati ya Pamoja ngazi ya Makatibu Wakuu kilichofanyika Mei 6, 2026 katika Kituo cha Huduma cha Pamoja Mpakani (OSBP) mjini Tunduma.
Kikao hicho cha Makatibu Wakuu kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Aristides Mbwasi (kwa upande wa Tanzania) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Bi. Lillian S. Bwalya (Mwenyekiti menza kwa upande wa Zambia).
Mbwasi ameongeza kuwa kikao hicho ni cha maandalizi kuelekea Mkutano ngazi ya Mawaziri unaotarajiwa kufanyika Mei 7, 2026, ukilenga kuimarisha zaidi ushirikiano wa uchumi, Biashara na Uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili jirani.
Katika kikao hicho, Makatibu Wakuu walipokea, kujadili na kupitisha mapendekezo pamoja na ajenda mbalimbali zilizowasilishwa na Mkutano wa Ngazi ya Wataalamu uliofanyika Mei 4 hadi 5, 2026.
