Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kamati ya Bunge yapongeza uendelezaji wa Kiwanda cha KMTCL




Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati na Kielelezo ya Liganga Mchuchuma, Magadi soda na ufufuaji wa Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited yenye maslahi makubwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) wakati wa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwasilisha Taarifa ya UTENDAJI WA Kiwanda cha KMTC Manufacturing Limited kilichosajiliwa Kampuni Tanzu ya NDC mwezi Machi, 2023 kilichojulikana kama Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ili kufanya kiwanda kujiendesha kibiashara kwa Kamati hiyo Januari 29, 2024 katika ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa KMTC ili kiweze kujiendesha wenyewe, kuongeza wigo wa utoaji huduma zake kuanzia kwenye viwanda hadi kwenye migodi ili kusaidia viwanda vingi vinavyohitaji vipuri na kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza vipuri nje ya Nchi.

Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara Bw. Needpeace ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara yake itayafanyia kazi maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kushirikiana na Kamati hiyo katika kuhakikisha Kiwanda hicho cha msingi kinachotengeneza vipuri kwa ajili ya viwanda vingine kinafanya kazi kwa tija na ufanisi katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania hususani wamiliki wa Viwanda kupenda kununua na kitumia vipuri mbalimbali vya zinazotengenezwa na KMTC ili kukilinda na kuviwezesha kuendelea na uzalishaji, kuongeza ajira, Pato la Taifa na kuendeleza Viwanda na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe akitoa elimu kwa wajumbe hao ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuiwezesha NDC kut