Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

KAPINGA AHIMIZA UZALISHAJI BIDHAA BORA VIWANDANI KUONGEZA AJIRA


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Judith Kapinga (Mb), ametoa wito kwa wazalishaji na wawekezaji kuendelea kuimarisha uzalishaji wa bidhaa bora nchini ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.

Akizungumza waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam , Desemba 18, 2025, Waziri Kapinga amesema uzalishaji wa ndani ni nguzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa taifa na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Ameeleza kuwa sekta ya viwanda inaendelea kuimarika, huku baadhi ya viwanda vya saruji, marumaru na mabati vikiongeza kiwango cha uzalishaji na kusambaza bidhaa kwa wingi sokoni.

Aidha, Waziri Kapinga amesema Serikali inaendelea kuweka sera na mikakati itakayopunguza changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa nishati, gharama za malighafi na changamoto katika usambazaji wa bidhaa ili kurahisisha shughuli za biashara.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na wajasiriamali wadogo, akibainisha kuwa uwekezaji katika uzalishaji wa ndani utatoa fursa zaidi za ajira kwa vijana na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Kwa upande mwingine, amezitaka mamlaka za idhibiti kushirikiana kwa karibu na wajasiriamali ili kuhakikisha bidhaa zinazalishwa kwa kiwango kikubwa huku zikizingatia viwango vya ubora na usalama wa watumiaji, hatua itakayosaidia kuongeza pato la taifa na kukuza biashara za ndani.