Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

KAPINGA: TUTAWAWEZESHA KURASIMISHA BIASHARA ZENU


Serikali imeahidi kuwawezesha Wafanyabiashara hususani Wanawake na Vijana kurasmisha biashara zao na kufanya kwa kuweka mazingira rafiki ya kukuza shughuli zao kiuchumi, kuondoa vikwazo vya urasimu, kama vile mlolongo mrefu wa kupata leseni na ithibati ya ubora, ili kuwawezesha wafanyabiashara wote, hususan wanawake na vijana, kufanya kazi kwa njia bora na endelevu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb.) wakati akihutubia katika hafla ya Women in Balance Kitchen Party Gala 2026 iliyofanyika Aprili 12, 2026, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Waziri Kapinga alieleza kuwa wafanyabiashara wasio na leseni au ithibati hawatafungiwa biashara zao, bali watapewa mwongozo na msaada wa kukamilisha taratibu muhimu, akisema, "Zama za kufungia biashara zimekwisha, sasa tunawawezesha.

Kapinga pia amewahimiza Wanawake kuchamkia fursa zilizopo na kurasimisha biashara zao ili kuchangia katika maono ya Taifa ya miaka 25 ijayo, ambapo sekta binafsi inategemewa kubeba asilimia 70 ya uchumi.