Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya laleta mafanikio makubwa katika uwekezaji na ufanyaji biashara nchini.


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya lilofanyika Februari 23  - 24/ 02/ 2023 limeleta mafanikio makubwa katika uwekezaji na ufanyaji biashara nchini kwa kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili kukutana na kukubaliana kuendeleza na biashara zao.

Ameyasema hayo 24 Februari, 2023 wakati akiongea na waandishi wa habari  baada ya  hafla ya kufunga Kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano JNICC, Dar es salaam.

Amesema Kongamano hilo ni moja ya matokeo ya Ziara  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasani  aliyoifanya katika nchi za  Umoja wa Ulaya  kwa lengo la kuifungua Tanzania kwa uchumi wa dunia.

Aidha, amesema  Serikali iko tayali kiwapokea wawekezaji na wafanyabiashara kutoka  Umoja wa ulaya kwa kuwa imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  ikiwemo kurekebisha sheria ikijumuisha Sheria ya uwekezaji ya 2022, kufuta baadhi ya tozo faini na ada, kuboresha matumizi ya mifumo ya tehama katika utoaji huduma kwa gjarama nafuu na muda mfupi na sheri

Aliongeza kuwa Kongamano hilo limefanikisha kusainiwa mikataba yenye thamani ya Euro bilioni 1, kati ya Benki za Umoja wa Ulaya na Benki za Tanzania ( EIB na CRDB,  NMB KCB ) ambapo  fedha zitakopeshwa kwa wanawake na vijana pamoja na uendelezaji wa uchumi wa bluu ambazo zitaongeza mapato , ajira na maendeleo ya kiuchumi na kijamii Tanzania.

Naye, Katibu Mkuu  - Uchumi na Uwekezaji - Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji  Dkt. Habiba Hassan Omar, amesema Serikali ya Zanzibar imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji  kwa kuboresha sheria ya biashara ambayo imefanyiwa marekebisho hivi karibuni.

Aidha, aliongeza kuwa Serikali ya Zanzibar inawakaribisha wawekezaji katika sekta za uvuvi wa bahari kuu, uvunaji wa mwani, uvunaji wa majongoo bahari, utalii wa bahari, ujenzi wa makazi ya bei nafuu ili kupunguza ujenzi holela katikia mji huo.

Naye Balozi w Umoja wa Ulaya nchini  Tanzania Mhe. Manfredo Fanti  amesema amefurahishwa na majadiliano yaliyofanyika kati ya Tanzania na wawekezaji kutoka  EU ambao umeiongezea Tanzania fursa nyingi za uwekezaji.