Habari
Maonesho ya Madini Geita kuwa ya Kimataifa

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu amesema kuwa kutokana na mwitikio mkubwa wa washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ipo haja ya kuyapandisha maonesho hayo nakuwa maonesho ya kimataifa ili kushirikisha nchi mbalimbali zitakazowawezesha wajasiriamali nchini na wadau katika sekita ya madini kuweza kuonesha bidhaa zao pamoja na kupata masoko ya kimataifa.
Bwana Gugu ameyasema hayo Oktoba 4, 2022 katika viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita alipo[1]tembelea mabanda mbalimbali ya Wajasiriamali na Sekta za Umma katika maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini nakujionea jinsi washiriki wamaonesho hayo walivyotumia fursa hiyo kuonesha bidhaa zao pamoja na ubunifu mbalimbali katika sekta ya madini.
Amesema maonesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini yakipewa hadhi yakuwa maonesho ya kimataifa yatawasaidia wajasiriamali pamoja na wadau katika sekita ya madini kuweza kutoka na kuuza huduma zao na bidhaa nje ya nchi. Maonesho haya yanawawezesha wajasiriamali kukuza kipato chao pamoja na kupata fursa ya kukutana na taasisi mbalimbali za kibenki zitakazo wasaidia kwa kuwakopesha ili kuwawezesha kuongeza mitaji yao. Ameongeza Bw. Gugu.
Aidha, amewataka wachimbaji wadogo wa madini kutumia vema fursa ya uwepo wa maonesho hayo katika kujifunza teknolojia mpya za uchimbaji wa madini pamoja na uongezi wa thamani kwenye madini ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji katika shughuli zao. Amesema Serikali ina mpango wa kuyapandisha hadhi maonesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika mkoani Geita kuwa ya kimataifa ili kupanua wigo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya madini pamoja na wajasiriamali kupata uzoefu kutoka katika kimataifa ya kigeni.