Habari
NDC KUHAKIKISHA MIRADI YA KIMKAKATI NA KIELELEZO INATEKELEZWA KIKAMILIFU

NDC hakikisheni Miradi yote ya Kimkakati na Kielelezo inatekelezwa kikamilifu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo
ameliagiza Shirika la Taifa la Maendeleo(NDC) kuhakikisha miradi yote ya kimkakati na kielelezo ikiwemo Mradi wa Chuma wa Maganga Matitu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni utekelezaji wake unasimamia kikamilifu kwa manufaa ya Taifa.
Ameyasema hayo Julai 29, 2024, jijini Dar es Salaam alipotembelea NDC kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika hilo hususani usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kielezo ya Taifa.
Aidha, amelipongeza Shirika hilo kwa kazi nzuri inalolifanya katika kusimamia miradi ya kimkakati na kielelezo ya Taifa ambayo inalenga kuviwezesha viwanda kupata malighafi muhimu kama vile chuma magadi soda na nk kwa urahisi nchini na kupunguza uagizaji malighafi hizo nje ya nchi ili
kukuza viwanda na uchumi kwa ujumla
"NDC ni Shirika kubwa linategemewa na Taifa, ndio roho ya uchumi, tujue tuna dhamana kubwa, hivyo tutapambana pamoja kuhakikisha NDC inafanya vizuri tumsaidie Rais," alisema Dkt. Jafo.
Aidha, ametoa wito kwa Watumishi wa Shirika hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, ubunifu na ushirikiano baina yao pamoja na ili kuendeleza Shirika hilo muhimu na kutimiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kujenga uchumi shindani wa viwanda.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NDC Dkt Nicholaus Shombe akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo amesema Shirika hilo linasimamia miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Liganga na Mchuchuma, Mradi wa chuma wa Maganga matitu na Magadi soda wa Engaruka
Aidha akielezea Mradi wa Chuma wa Maganga Matitu ambao Mkataba wake na Mwekezaji unasainiwa hivi karibuni ambapo mwekezaji atakuwa na asilimia 64 na Serikali 36
unatarajiwa kuanza kuchimba kiasi cha tani milioni moja kwa mwaka na uzalishaji utaongezeka