Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Taasisi zote za umma ambazo hutoa huduma kwa wateja zatakiwa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.)amezitaka Taasisi zote za umma ambazo hutoa huduma kwa wateja kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji hao kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na weledi mkubwa ili kuepukana na uharibifu wa Mazingira

Kigahe ameyasema hayo Septemba 22, 2023 alipokuwa akishiriki Kikao kazi cha watoa huduma za leseni zinazohusiana na uchimbaji na uwezeshaji mitaji katika ukumbi uliopo katika Viwanja vya Maonesho ya Sita (6) ya Teknojia ya Madini Geita.