Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMEAMUA KUENDELEZA AJENDA YA VIWANDA KWA KASI ZAIDI


Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amewahakikishia wenye viwanda na wafanyabiashara kuwa Serikali ya awamu ya sita imeamua kuendeleza ajenda ya viwanda kwa kasi na mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji yanendelea kuboreshwa Zaidi.

 

Prof. Mkumbo ameeleza hayo leo Disemba 14, 2021 wakati akiweka jiwe la msingi na kuzindua kiwanda cha mabati cha Epic Roofing Sheet Manufafacturing Co. Ltd kilichopo Shekilango Dar es salaam.

 

“Niwahakikishie wenye viwanda na wafanyabiasha kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan tumeamua kuendeleza ajenda ya viwanda kama ilivyokuwa awamu ya tano na sasa mazinigira ni mazuri Zaidi” amesema Prof. Mkumbo

 

 

Prof. Mkumbo amesema hapa Tanzania viwanda vimetengwa katika vipaumbele vitatu ambapo cha kwanza ni viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kipaumbele cha pili ni viwanda vya kutengeneza na kuzalisha bidhaa za nguo na mavazi, cha tatu ni viwanda vinavyozalisha bidhaa na vifaa vya ujenzi.

 

Aidha, Prof. Mkumbo ameeleza kuwa kiwanda cha mabati kitasaidia na kuongeza bidhaa za mabati  kwa kipindi hiki ambacho yanahitaji sana kutokana Watanzania wengi wamehamasika wa kujenga.

 

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Epic, Epimack Makoi ameeleza kuwa kiwanda kimejitahidi kusimamia ubora wa bati kwa kuhakikisha Watanzania wanapata bidhaa bora kwa ajiri ya kuezekea nyumba zao kwa kutambua kuwa nyumba bora ni moja ya hitaji muhimu la binadamu.

 

Vilevile, Eoimack Makoi ameeleza changamoto ambazo zinakumba sekta ya viwanda ambazo ni kukosekana umeme wa uhakika viwandani na changamoto ya nguvukazi ya wafanyakazi kutokana na ujuzi unatoakiwa kwenye soko la ajira  na ukuaji wa teknogia

 

Kiwanda cha Mabati cha Epic kimeanza kufanya kazi mwezi Februari 2021 na kina wafanyakazi kumi na nne wa kudumu na vibarua 10