Habari
TANTRADE endeleeni kuboresha mazingira ya biashara, uwekezaji, utoaji wa huduma na jitihada za utafutaji wa masoko ya nje kwa ajili ya bidhaa za Tanzania.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji( Mb.) amekutana na kujadiliana na Menejimenti ya Mamlaka ya Maendeleo Biashara Tanzania (TANTRATE) Januari 24, 2023 kuhusu uboreshaji wa mazingira ya biashara, uwekezaji, utoaji wa huduma na jitihada za utafutaji wa masoko ya nje kwa ajili ya bidhaa za Tanzania.