Habari
TANZANIA NA UINGEREZA KUIMARISHA UHUSIANO WA BIASHARA, VIWANDA NA UWEKEZAJI
Tanzania na Uingereza zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa biashara, viwanda na uwekezaji kwa kuongeza juhudi za kuelimisha jamii ya wafanyabiashara kuhusu Mpango wa Biashara wa Uingereza kwa Nchi Zinazoendelea (Developing Country Trading Scheme - DCTS).
Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith S. Kapinga (Mb), na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. Marianne Young, yaliyofanyika Januari 28, 2026, katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
Aidha, viongozi hao walijadili uendelezaji wa ushirikiano katika Biashara Mtandao (e-commerce) ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani na kukuza zaidi kiasi cha biashara kati ya nchi hizi mbili.
