Habari
Tanzania ina Mazingira Bora ya Uwekezaji na Ufanyaji Biashara

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ikiwemo Aridhi, Amani na malighafi za kutosha hususani gesi asilia kwa viwanda vya utengenezaji wa mbolea.
Ameyasema hayo Oktoba 11, 2022 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Indorama Com merce DMCC ya India Bw. Venkatesh Gopalan na ujumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam.
Wakijadiliana kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania Bw. Gopalan amesema Kampuni yake iko tayali kuja kiwekeza Tanzania hasa katika viwanda vya kutengeneza Mbolea kwa kutumia gesi asilia, sekta ya kilimo na madini.