Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania kuuza Mbolea ya Intacom Uganda.


Tanzania kuuza Mbolea ya Intacom Uganda.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema fursa ya Tanzania kuuza mbolea inayotengenezwa na Kiwanda kinachozalisha mbolea asilia cha Intracom Fertilizer limited IFL nchini Uganda kutaongeza ajira, Pato la Taifa, kukuza uchumi na uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Uganda.

Ameyasema hayo Januari 29, 2025 wakati aliposhiriki ziara ya Waziri Mkuu wa Uganda Mhe Robinah Nabbanjah aliyekuja kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Nishati- M300 alipotembelea Kiwanda hicho na kuonyesha kuridhishwa na uwekezaji huo katika Kiwanda hicho cha ITRACOM kinachozalisha mbolea asilia ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kulinda afya ya udongo.

Aidha, Waziri Jafo amesema Kiwanda hicho kilichoanza kuzalisha mbolea tani 200000 kwa mwaka na kwa sasa kinauwezo wa kuzalisha tani 800,000 kwa mwaka na kinapanga kuongeza uzalishaji tani 1000,000 kwa mwaka kwa sasa kinauwezo wa kuzalisha mbolea kwa mahitaji ya ndani na nje ya nchi.

Aidha amefafanua kuwa uuzaji wa mbolea hiyo nchini Uganda ni moja ya utekelezaji wa makubaliana ya kufanya biashara ndani ya ncxhi za Afrika Mashariki na Mkataba wa Eneo huru la Biashara Afrika (AfCFTA)

Vilevile Dkt Jafo amefafanua kuwa Kiwanda hicho kinachotoa ajira ya moja kwa moja 827 kinazalisha aina kumi za mbolea ikiwemo FOMI Otesha, FOMI Kuzia, FOMI Nenepesha, CHOKAA Kilimo, FOMI Chai+, FOMI Chai++, FOMI Cans, FOMI Junia and FOMI Supa kitaongeza uzalishaji na ajira zaidi kitakapoendelea kupanua uzalishaji na kuongeza mauzo ya mbolea hizo ndani na nje ya nchi.