Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania na Marekani kukuza uhusiano wakibiashara


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na
kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi "Mission Director" wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Bw. Craig Hart kuhusu kukuza biashara kati ya Tanzania na Marekani, Novemba 06, 2023 jijini Dar es Salaam.


Aidha, Waziri Kijaji amempongeza Bw. Craig kwa mchango wa Shirika hilo katika kufanikisha Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) na amemsihi kusaidia Vijana kupata masoko ya bidhaa zinazozalishwa kupitia Mpango huo wa BBT.