Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania Yazindua Kiwanda Kikubwa cha Vioo Afrika Mashariki na Kati


Tanzania Yazindua Kiwanda Kikubwa cha Vioo Afrika Mashariki na Kati

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema uzinduzi wa kiwanda kikubwa cha vioo Afrika Mashariki na Kati ni hatua muhimu katika kuendeleza sekta ya viwanda nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Septemba 20, 2023 Mkuranga, Pwani, Waziri Kijaji amesema uzinduzi wa Kiwanda hicho moja wapo wa viwanda vinne vya kutengeneza Vioo Barani Afrika ni ushindi mkubwa kwa Tanzania kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Kiwanda cha Sapphire chenye uwezo wa kuzalisha tani 400,000 za vioo kwa mwaka na
kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 1,650 na zisizo za moja kwa moja 6,000

Pia, amebainisha kuwa Kiwanda hicho kinatarajiwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na dolomite, silca sand, limestone, feldspar pamoja na magadi soda yanayopatikana Engaruka na kinatarajia kuuza bidhaa zake katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Serikali ya awamu ya sita ina dhamira ya dhati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini," alisema Waziri Kijaji. "Tutaendelea kutoa mazingira mazuri kwa wawekezaji ili waweze kuwekeza nchini Tanzania."

See translation