Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI YAWAFUNDA WATUMISHI WAPYA WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA


Watumishi 32 walioajiriwa Wizara ya Viwanda na Biashara mwezi Mei na Agosti, 2025 wamepewa Mafunzo Elekezi ya kuwajengea uwezo wa kuendelea kuboresha utendaji kazi wa kuwahudumia wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa siku tatu, yametolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, tawi la Singida Oktoba 22 hadi 24, 2025 jijini Dodoma.