Habari
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC yaipongeza Wizara*
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma PIC yaipongeza Wizara*
Wizara ya Viwanda na Biashara imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya Wakala wa Vipimo WMA
Pongezi hizo zimetolewa Machi 13, 2025 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Augustine Vuma wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya WMA Makao Makuu iliyopo Medeli jijini Dodoma.
Aidha, Mhe. Vuma amesema kuwa, Kamati yake imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo la kisasa ambalo limejengwa na Mkandarasi mzawa na kusaidia kutoa fursa kwa wasomi na wataalamu wa ndani ambao wamesaidia tengeneza ajira kwa Watanzania na kuanza kujivunia vyakwetu.
Amesema kuwa, kukamilika kwa jengo hilo ni moja ya kutekeleza maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita yaliyotolewa kwa Serikali na Taasisi zake zote kuhamia Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abadlah akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ulianza tarehe 02 Julai 2022 huku ujenzi wake ukitarajia kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 5.8
Dkt. Hashil ameeleza kuwa , wakati wa ujenzi wa jengo hilo baadhi ya kazi ziliongezeka ambazo hazikuwepo kwenye Maktaba wa awali na kufikia bilioni 6.9 ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.81
Amesema kuwa ,Jengo hili ambalo ndipo yalipo Makao Makuu ya Wakala wa Vipimo nchini WMA lina urefu ghorofa 5 ,vyumba 60 vya ofisi maabara moja ukumbi wa Mkutano wenyewe uwezo wa kuhudumia watu 100 na sehemu ya kupaki Magari.
Dkt Abadlah amezitaja faida za kukamilika kwa jengo hilo linalojengwa na Mkandarasi mzawa Ms.Mohamed Builders Ltd kuwa kutasaidia ari ya utendaji kwa wafanyakazi wa WMA kutokana na kufanya kazi katika mazingira mazuri ,pia kutaongeza motisha kwa wafanyakazi na kupunguza gharama za kulipa kodi ya pango kwenye majengo binafsi.