Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Ushirikiano uliopo baina ya Japan na Tanzania katika shughuli mbalimbali za maendeleo ni wa muda mrefu.


Katibu Mkuu Dkt. Hashil Abdallah amekutana na kufanya Mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa JICA nchini Tanzania Bw. Ara Hitoshi

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya Japan na Tanzania katika shughuli mbalimbali za maendeleo ni wa muda mrefu na wenye mafanikio hasa katika sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kupitia utekelezaji wa mradi wa KAIZEN awamu ya tatu unaojulikana kama Business Development Services (BDS) ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka minne (4) kuanzia mwezi Mei, 2023 hadi Mei, 2027.

Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa JICA katika ofisi ya Tanzania Bw. Ara Hitoshi amesema kuwa anashukuru kwa ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Japan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Japan kupitia JICA. 

Bw. Hitoshi ameongeza kuwa mradi wa KAIZEN awamu ya tatu umejikita zaidi kutoa huduma katika viwanda vinavyotekeleza dhana ya KAIZEN kwa Tanzania bara na Tanzania Visiwani.