Habari
WANAWAKE WAKIFANIKIWA KATIKA BIASHARA KUNA UWEZEKANO WA KUVUNJA MNYORORO WA UMASIKINI
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa wanawake wakifanikikwa katika biashara kuna uwezekano mkubwa wa kuvuja mnyororo wa umasikini katika familia na Taifa kwa ujumla.
Prof. Mkumbo alieleza hayo Disemba 04, 2021 wakati akiongea katika kongamano la Wanawake na kikoba wa kikundi cha Women of hope alive lililofanyika Mlimani City vilevile katika kongamano la 4 la Women in bussines connet gall 2021 lililofanyika Ubungo plaza Dar es salaam.
“Njia moja rahisi ya kuvunja mnyororo wa umaskini ni wanawake kufanikiwa katika biashara, wanawake wakifanikiwa inawezekana katika Taifa hilo likavunja mnyororo wa umasikini kwa sababu asilimia 90 ya mapato yao hutumika kwenye vitu vinavyofaidisha familia moja kwa moja”
Prof. Mkumbo alitoa wito kwa wanawake kujiamini katika shughuli wanazozifanya katika jamii na kujifunza kumiliki mafanikio wanayoyapata huku awataka kujifuza katika mfano bora kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni moja wa kiongozi mwanamke mahili duniani.
Aidha, wakati akijibu risala ya kongamano la wanawake na kikoba, Prof. Mkumbo aliwaagiza TBS kupitia mpango wao maalum wa kutoa elimu kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kuwapa elimu wanawake namna ya kupata nembo ya idhabiti na kuzalisha bidhaa bora vilevile EPZA watoe elimu bure namna ya kukidhi matakwa ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi.
kongamano la Wanawake na kikoba wa kikundi cha Women of hope alive hufanyika mara moja kila mwaka kwa lengo mahususi la kuwakutanisha wanavikoba wote kutoka Mkoa wa Dar es Salaam wenye nia moja ya kuhakikisha Mwanamke anajikwamua kiuchumi na kuzitumia vizuri fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa wetu wa Dar es Salaam.
Vile vile, kongamano la 4 la Women in bussines connet gall 2021 liliwakutanisha mama wajasiriamali na wafanyabiashara kwa madhumuni ya kubadilisha uzoefu, kupeana ujuzi na mwelekeo ili kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuwa vinara katika Maendeleo.