Habari
Watanzania wametakiwa kuvilinda viwanda vya ndani ya nchi
Watanzania wametakiwa kuvilinda viwanda vya ndani ya nchi na kupenda kununua na kitumia bidhaa zinazotengenezwa na viwanda hivyo ili kuvilinda na kuviwezesha kuendelea na uzalishaji, kuongeza ajira, pato la Taifa na kukuza uchumi kwa ujumla
Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kulinda viwanda vya Serikalli kwa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, uzalendo na hofu ya Mungu ili kiepuka kusababisha uharibifu unaoweza kutokea kwa kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kuvifufua na kuviendesha viwanda hivyo.
Ameyasema hayo Agosti 23, 2024 wakati wa Ziara yake Mkoani Kilimanjaro ambapo alipotembelea viwanda, kuongea na Wafanyabiara pamoja na Maafisa Biashara wa Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughjuli za uzalishaji, kusikiliza changamoto na kuona njia bora ya kuzitata kwa kushirikiana na Taasisi nyingine husika.
Aidha, Waziri Jafo akiwa mkoani humo alitembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vinywaji baridi cha Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd, Kiwanda cha Bonite Bottlers Ltd, Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro, Kiwanda cha kutengeneza vipuri na mitambo mbalimbali cha KMTC, Eneo la uwekezaji la bustani ya wanyamapori ya Serval (Serval Wildlife) pamoja na Kiwanda cha Sukari Moshi (TPC).
Akiwa katika Eneo la uwekezaji la bustani ya wanyamapori ya Serval (Serval Wildlife) Dkt. Jafo amewahimiza Watanzania kutumia muda wao wa mapumziko kufanya utalii wa ndani ili kukiza biashara ya utalii na kuvutia wafanyabiashara katika sekta hiyo ilo kukuza biashara
Katika hatua nyingine akiongea na Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda wa Mkoa wa Kilimanjaro, Waziri Jafo amewataka Watumishi wa Umma Mkoani humo kiwasaidia wafanyabiashara na amewaahidi kuwa atashirikiana na Taasisi nyingine za kisekta kutatua changamoto zilizopo na kwa lengo la kuendelea kuweka mazingira bora ya biashara kwa kupunguza gharama za uendeshaji ili kuvutia uwekezaji na ufanyaji biashara nchini
Vilevile Dkt Jafo amehamasisha utrkelezaji wa Mpango wa Viwanda Tqnzankq unaoelekeza kuwa kila Mkoa unapaswa kuanzisha Viwanda vikubwa 3, Viwanda vya kati 5, Viwanda vidogo 20 na Viwanda vidogo sana 30 ili kukukuza sekta ya viwanda kuongeza ajira na pato la Taifa