Habari
WAZIRI PROF. MKUMBO AFANYA MAZUNGUMZO YA KUIMALISHA USHIRIKIANO NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA LA UMOJA WA MATAIFA (UNIDO)

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila A. Mkumbo leo tarehe 04 Agosti 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) Dkt. Stephen B. Kargbo katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimalisha ushirikiano kati ya Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Shirika hilo. Pia Kikao hicho kimehusisha Timu ya Wataalam ya Wizara ya Wizara ya Viwanda na Biashara inayoandaa Mwongozo wa Mitaa ya Viwanda (Industrial Parks) na Mgawanyo wa Viwanda (Classification of Industries in Tanzania), hatua zinazolenga kuimalisha Sekta ya Viwanda ili iweze kuwa chachu ya maendeleo ya ukuaji uchumi kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa FYDP III.
Katika Kikao hicho Mheshimiwa Waziri ametoa shukrani za Serikali kwa hatua mbalimbali za ushirikiano katika eneo la kukuza viwanda zinazofanywa na UNIDO na kuhimiza umuhimu wa pande zote mbili kushirikiana kwa karibu katika kuandaa Mwongozo wa Kuendeleza na Kusimamia Mitaa ya Viwanda ili uwe chachu ya kukuza sekta hiyo nchini.