Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Bashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali itaenda hatua kwa hatua kuhakikisha changamoto wanazopata wenye viwanda zinatatuliwa na kushughulikiwa kwa wakati


Waziri wa Viwanda na Bashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali itaenda hatua kwa hatua kuhakikisha changamoto wanazopata wenye viwanda zinatatuliwa na kushughulikiwa kwa wakati

Dkt. Kijaji amesema hayo Julai 26,2023 alipotembelea Kiwanda  cha Mbolea ITRACOM  kilichopo Nala Jijini, Dodoma kujionea uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho.

Aidha Amekipongeza  Kiwanda hicho kwa utengenezaji wa mbolea usiokua na mchanganyiko wa asilimia 100 ya madini, bali asilimia 50 ni samadi na asilimia 50 ni madini ambao unaleta  uhai wa ardhi kwa uasili na ubora wake 

Amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi  wa Kiwanda hicho kwa awamu ya kwanza, kitaweza kuzalisha  Tani millioni 1.2 kwa mwaka  huku matumizi ya ndanj ya nchi ni Tani 650,000 hivyo hakuna sababu yakuagiza mbolea nje ya nchi

Aidha Dkt. Kijaji amesema amezikaribisha nchi za Afrik Mashariki na Afrika kwa ujumla  ikiwemo kenya ambayo tayari imeshanunua  tani 3000 za mbolea kununua mbolea kutoka ITRACOM  Mbolea ya  Dodoma Tanzania

Naye Mkurugenzi wa ITRACOM Bw Nduwimana Nazaire ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutambua juhudi za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho na ameiomba  Wizara ya Viwanda na Baishara kushirikiana na Wizara zingine katika juhudi za usambazaji wa mbolea hiyo.