Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

BALOZI WA CUBA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI OFISINI KWAKE

Balozi wa Cuba nchini leo amemtembelea Mhe. Waziri ofisini kwake. Balozi huyo ambaye aliongozana na maafisa kadhaa toka ofisi za Ubalozi amefanya ziara hiyo kwa lengo la kutoa salam za Mwaka Mpya na Pia kutoa hongera kwa Mhe. Waziri kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Viawanda, Biasharana Uwekezaji katika Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. John Pombe, Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi amemtembelea Mhe. Waziri kuelezea pia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Kiwanda cha Viuadudu kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe Balozi alielezea hatua nzuri iliyofikiwa na kwamba kiasi cha fedha kilichobaki ambacho Serikali yetu bado haijakitoa ndio imekuwa kikwazo cha kuanza kwa uzalishaji wa dawa hizo. Kwa upande wake, Mhe. Waziri alifurahi kutembelewa na Balozi huyo na kumhakikishia ushirikiano wa kutosha katika kipindi hiki na kwamba atadumisha ushirikiano uliokuwepo kati ya Tanzania na Cuba tangu Uhuru. Kuhusu fedha ambazo bado hazijatolewa na Serikali kupitia NDC, Mhe. Waziri ameahidi kulifuatilia suala hilo ili fedha hiyo iweze kutolewa mapema isicheleweshe kuanza kwa uzalishaji wa dawa hiyo kwani ugonjwa wa Malaria ndio unaoongoza kwa kusababisha vifo hapa nchini na nchi zingine za Afrika.